Mratibu
wa taifa wa utepe mweupe wa Uzazi salama Tanzania Dkt. Rose Mlay
akiwasilisha mada iitwayo “Wajibika Mama Aishi” katika Mkutano na
viongozi wa idara ya afya pamoja na wadau wa Sekta hiyo Mkoani Rukwa
katika ukumbi wa RDC tarehe 21 Oktoba 2013 kujadili matumizi bora ya
bajeti zilizowekwa na kuzipa kipaombele katika kusaidia uhai wa mama
wajawazito katika vituo vya afya Mkoani Rukwa. Akielezea lengo la
taasisi hiyo ya “White Ribbon” alisema ni kuimbusha Serikali ya Tanzania
kutekeleza ahadi yake ya kuwa na asilimia hamsini ya vituo vya afya
Mkoani Rukwa vitakavyotoa huduma kamili za dharura za uzazi zikiwa ni
pamoja na upasuaji kumtoa mtoto na kutoa damu salama zinapohitajika
ifikapo 2015.
Mganga
Mkuu Hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akitoa maelezo
mafupi juu ya huduma za kinamama wajawazito Mkoani Rukwa katika Mkutano
huo. Alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya Mkoani
Rukwa ni uhaba wa watumishi katika sekta ya afya, uhaba wa magari ya
wagonjwa kuweza kuwasaidia wananchi waliombali na huduma za afya pamoja
na Vituo vingi vya afya na zahanati kutokuwa na vyumba vya upasuaji
hususani katika maeneo ya mwambao na maeneo mengine ya pembezoni. Kulia
ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Kushoto ni Mratibu wa taifa wa utepe mweupe wa Uzazi salama Tanzania Dkt. Rose Mlay.
Baadhi
ya watumishi wa idara ya afya Mkoani Rukwa na wadau wengine wa sekta
hiyo wakisikiliza uwasilishwaji wa mada mbalimbali katika Mkutano huo.
Shirika la Utepe Mweupe Tanzania “White Ribbon Alliance for Safe
Motherhood in Taznania(WRATZ)” linaendeleza kampeni yake ya miaka mitatu
iitwayo “Wajibika Mama Aishi” (Be Accountable sa Mama can Survive
Childbirth) kwa kuendesha mikutano na Semina mbalimbali kwa wadau wa
afya katika ngazi ya Serikali na kijamii katika maeneo mbalimbali hapa
nchini; Lengo kuu likiwa kuikumbusha Serikali juu ya utekelzaji wa ahadi
yake ya kuboresha huduma kamili za dharura za uzazi zikiwa ni pamoja na
upasuaji kumtoa mtoto na kutoa damu salama zinapohitajika ifikapo 2015.
Ahadi hiyo kwa kiasi kikubwa inaendelea kutekelezwa na Serikali ya
awamu ya nne na ifikapo mwaka 2015 itakuwa kipindi cha kuifanyia
tathmini.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment