HATUA ZA MWISHO ZA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA KLABU YA SOKA YA SUNDERLAND YA UINGEREZA ILI KUWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA SEKTA YA UTALII PAMOJA NA KUINUA SOKA NCHINI. Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland, Bw. Gary Hutchinson (wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua ya mazungumzo waliyofikia kujenga kituo cha michezo katika Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua mchezo wa mpira wa miguu. (wakwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Michezo Nchini Bw.leonard Tadeo, (wapili kulia) Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki, (wakwanza kushoto) ni Mwakilishi wa klabu ya Sunderland Tanzania,Bw Edmund Hazzad. Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland Bw Gary Hutchinson, (kushoto) akimkabidhi mkurugenzi wa wizara ya Habari, Vijana, utamaduni na michezo Bw. Leonard Tadeo jezi ambayo imesainiwa na wachezaji wa sunderland Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland, Bw Gary Hutchinson, Tisheti ya Bodi ya Utalii. Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali walioudhuria kwenye mkutano huo. Picha Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment