MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekosa
penalti kwa mara ya kwanza maishani mwake wakati AC Milan ikilala 2-1
nyumbani katika mchezo wa Serie A dhidi ya vinara Napoli Jumapili hii.
Balotelli, ambaye amefunga penalti zake
zote 21 za awali katika mechi rasmi, alishuhudia mkwaju wake ukiokolewa
na kipa Pepe Reina dakika ya 60.
Hata
hivyo, 'Supermario' aliifungia Milan dakika ya 90 na ushei kabla ya
kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje miwishoni mwa mchezo. Mabao ya Napoli yalifungwa na Britos dakika ya sita na Higuaín dakika ya 54 pasi ya Zuniga.

Nyekundu: Mario Balotelli, kuahoto akitulizwa na mchezaji mwenzake wa Milan, Marco Amelia baada ya kulimwa kadi nyekundu


Kachaa Mario: Baloteli akibishana na refa Luca Banti

Anakosa: Mario Balotelli akikosa penalti

Kaokoa: Pepe Reina ameokoa penalti ya Balotelli

Amefunga: Gonzalo Higuain ameifungia timu yake mpya

La pili: Miguel Britos akiifungia Napoli bao la pili

Pigo takatifu: Balotelli akifunga kwa tik tak
0 comments:
Post a Comment