Monday, July 22, 2013


ashanti7Na Baraka Mpenja 
Wauza Mitumba wa Ashanti United ama watoto wa jiji, wanatarajia kuondoka kesho kutwa kuelekea Mkoani Kigoma ambako watakaa chimboni kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaorajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Abubakar Sellasi ameiambia MATUKIO DUNAINI kuwa wameamua kwenda mkoani ili kujifua kwa amani na utulivu kwani mjini nako kuna mambo mengi sana yanayoweza kuwaondolea umakini wachezaji wao.
“Mjini Kuna fitina nyingi na mambo mengi ya starehe kwa wachezaji, wewe si unajua soka letu bwana, tunaenda kujichimbia kigoma ili kujipanga zaidi. Tunajua wazi kuwa ligi kuu itakuwa changamoto mpya kwetu”. Alisema Sellasi.
Sellasi alisema mpaka sasa hawajaanza mazoezi rasmi, lakini walikuwa na program maalumu ya kusajili wachezaji wapya ambapo njia iliyotumika ni kuwaita wachezaji kufanya usaili mbele ya becnhi la ufundi na wale walioonekana kuwa na uwezo taratibu za kuwasajili zimeshaanza.
“Lengo letu ni kuwa na kikosi bora cha kushindana, Ashanti si timu ngeni, mimi nasema hivi: msimu wetu utakuwa mzuri sana kwani kambi ya Kigoma itakuwa kiboko”. Alisema Sellasi.
Sellasi alisema wanajitahidi kuwekeza zaidi katika soka la vijana, na lengo lao ni kuwa na uwezo wa kuwaendeleza vijana wao kwa maana ya kutoka timu B na kupandishwa timu A ili kuweka utamaduni mmoja wa klabu.
“Tunahitaji kuwa na falsafa ya Ashanti, kwa maana hiyo lazima tuwe na vijana wengi ambao watapandikizwa mbegu ya falsafa yetu. Tutatupia macho zaidi katika soka la vijana kuliko kuhangaika na wakongwe ambao umri umekimbia zaidi”. Alisema Sellasi.
Ashanti ambao hivi karibuni walifungwa mabao 5-1 dhidi ya Azam fc katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Chamazi, Mbande, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, watacheza msimu ujao wa ligi kuu baada yakufanikiwa kukata tiketi msimu uliopita wa ligi daraja la kwanza.
Klabu nyingine mbili zilizopata nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao ni Mbeya City kutoka jijini Mbeya, na maafande wa Jeshi wa Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video