Tuesday, July 23, 2013


IMG_0818Na Baraka Mpenja 
Siku moja baada ya shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF kuanika hadharani ratiba nzima ya ligi kuu soka Tanzania bara, maafande wa jeshi la kujenga Taifa wenye makazi yao katika dimba la Mabatini Mlandizi mkoani Pwani , klabu ya Ruvu Shooting wametamba kuanza kwa kasi katika harakati zao za kuwania ubingwa ama nafasi ya pili na tatu.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI kutoka Pwani, Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa “Masta” anaendelea na progrmu nzuri ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu unaotarajiwa kuanza  kutimua  vumbi Agosti 24 mwaka huu  kwa timu zote kushuka dimbani.
Masau alisema wamefurahi kuanza uwanja wao wa nyumbani wa Mabatini dhidi ya maafande wa Magereza kutoka  jijini Mbeya “Wajelajela” Tanzania Prisons, mechi ambayo wanajiandaa kuchukua pointi tatu za kwanza.
“Tuko kambini muda mrefu sana, hakika vijana wako makini kusikiliza kocha Mkwasa anawaeleza nini. Malengo yetu yako wazi, tunataka kuchukua ubingwa na kama tutashindwa basi lazima tushike nafasi ya pili au tatu”. Alisema Masau.
Masau alisema wanachotaka kwa sasa ni kupeperusha bendara ya taifa michuano ya kimataifa, kwani wale wanaowakilisha wanafanya vibaya  na hii inaonesha wanashindwa kujipanga mapema.
“Simba na Yanga wamekuwa wakipokezana ubingwa kama mbio za vijiti, ni wakati wa mapinduzi, tunataka kuwakilisha Taifa michuano ya kimataifa. Si wao wameshindwa “. Alisisitiza Masau.
Pia Afisa habari huyo aliwaomba waamuzi watakaopangwa kuchezesha mechi  za ligi kuu wachezeshe kwa haki kwa maana ya kufuata sheria 17 za mchezo wa soka.
“Huwa tunaonewa sana, napiga kelele sana na watu wanadhani pengine ni maneni ya aliyefungwa, waamuzi wanatuonea sana, wakibadilika na kuchezesha kwa haki, tutafika mbali”. Alisema Masau.
Masau alisema kwa usajili wa nyota wakali wakiwemo Elias Maguli, Stephano Mwasyika na wengineo, lazima wafalme wa soka nchini Tanzania waone maluweluwe machoni kwao kwani watakimbizwa vibaya sana.
Mechi ya pili maafande hao watasafiri mpaka jijini Mbeya kucheza na timu mpya ya ligi kuu, Mbeya City katika dimba la Sokoine mnamo Agosti 28.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video