Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa soka nchini England, klabu ya Manchester United leo hii imefanya mazoezi mazoezi ufukweni mwa bahari ambapo walisafiri kutoka bandari ya Sydney kwenda Ufukwe wa Bondi kwa njia ya boti.
Mazoezi hayo yamefanyika katika bichi ya Bondi kabla ya kukwea pipa kuelekea nchini Japan kuendelea na ziara ya ya kujianda na msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
Vijana hao wa David moyes watakuwa na mechi tano za kirafiki nchini Japan na jumanne ya kesho kutwa watashuka dimbani kucheza na Yokohama F-Marinos mjini Yokohama.
Kufuatia ushindi wa mabao 5-1 walioupata jana dhidi ya A-League All Stars , kikosi hicho leo asubuhi kimefanya mazoezi fukwe za Bond.





Mapumziko: Giggs, juu, na Wilfried Zaha chini wakipumzika ufukweni


0 comments:
Post a Comment