

Baadhi ya wanafunzi waliofika katika banda la VETA wakipata maelezo kutoka kwa Theopista Michael ambaye ni mwanafunzi wa chuo VETA cha Njiro Arusha kinachotoa mafunzo ya Diploma ya mambo ya hoteli na utalii.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipewa maelezo na Mwalimu wa VETA Tabora Diana Mlengeki juu ya mashine ya useketaji wa nguo aina mbalimbali zitokanazo na nyunzi wakati alipofika katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali zinazotplewa na Chuo hicho katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi wakati alipotembelea katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment