






Picha Zote na Frank Shija – Maelezo
Na Frank Shija Maelezo
Vijana watakiwa kuwa na fikra za kimkakati ili kukabiliana na changamoto Zinazowakabili katika kupambana na umqasikini.
Rai hiyo imetolewa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokuwa akiwasilisha mada juu ya vijana kuwa na fikra za kimkakati katika kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Vijana kinachojulika kwa jina la Chimbo School of Thought jana jijini Dar es Salaam.
Profesa Ole Gabriel amesema kuwa inakuwa ni tatizo kwa vijana kupambana na changamoto za maisha kwakuwa vijana wengi hawaweki mikakati katika fikra zao.
“Vijana mnapaswa kubadilika na kuanza kuwaza na kupanga mambo yenu kimkakati maana hakuna kitu kinafanikiwa bila ya kuwekewa mikakati,nah ii ndiyo maana mmekuwa mkikumbana na changamoto mbalambali na kukata tama.” Alisema Profesa Ol Gabriel.
Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa takwimu zina onyesha takriban asilimia 35.1 ya idadi ya watu ni Vijana na ambapo vijana wanachua karibu asilimia 70 ya nguvu kazi,hivyo wasipo kuwa na fikra na kupanga mambo yao kimkakati nchi itapata hasara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Chimbo School of Thought Mchungaji Harris Kapiga amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa vijana kama nguvu kazi ya taifa kituo chake kimenuia kubadilisha vijana wengi nchini ili wawe na mitazamo chanya ili wajiletee maendeleo yao wenyewe.
Mchungaji Kapiga aliongeza kuwa kupitia kituo chake vijana wengi wamebadilika kimtazamo na kutoa wito kwa vijana wengi kushiriki katika makongamano mbalimbali yanayoandaliwa kwa ajili yao ili wajifunze na kupata ufahamu wa mambo mengi zaidi.
0 comments:
Post a Comment