Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Baada
ya mazungumzo baina ya kocha mpya wa Manchester United, David Moyes na
mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Wayne Rooney juu ya hatima yake katika
dimba la Old Trafford kugonga mwamba hapo jana, leo hii wawili hao
wamekutana tena na kuendelea na majadiliano yao.
Rooney
mwenye umri wa miaka 27, leo hii kwa mara ya kwanza ametokeza katika
mazoezi ya Manchester United ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu
nchini England, huku akiwa katika gari yake ya Gharama kubwa Range
Rover.
Jana
alikutana na Moyes kujadili hatima yake katika klabu ya United, lakini
hawakufikia muafaka, hivyo leo hii pia wana mazungumzo nyeti.
Leo hii Rooney alifika mazoezini na kutumia muda mfupi na baada ya hapo aliondoka katika uwanja huo wa mazoezi wa United uitwao Carrington majira ya mchana.
Msimu
uliopita nyota huyo alitofautiana na bosi wake Sir Alex Ferguson baada
ya kumuweka benchi katika mechi muhimu, pia ujio wa Robin Van Persie
ulimpotezea nafasi yake katika kikosi chake cha kwanza.
Klabu
za Asernal na Chelsea tayari zimeshaonesha nia ya kumsaka Roonye ili
kuimarisha vikosi vyao. Lakini tusubiri leo hii nini kitatoa katika
mazungumzo ya nyota huyo na bosi wake mpya David Moyes.

Amerudi:
Wayne Rooney alifika katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United wa
Carrington akiwa na mkoko wake wa nguvu aina ya Range Rover asubuhi ya
leo

Wanakutana chemba tena: Rooney na Moyes wanakutana tena kujadili hatima ya mchezaji huyo

Rooney akiendesha katika dimba la Carrington majira ya asubuhi akiwasili kufanya mazoezi
Wakati
hayo yakijili, naye mchezaji wa United, Mkongwe Rio Ferdinand
ameonekana kuwa mwenye furaha baada ya kurejea katika mazoezi ya
kujiandaa na msimu mpya akiandika katika mtandao wake wa Twita kuwa
“Siku yangu ya kwanza kujiandaa na msimu mpya, siku ya kwanza
kutengeneza mafanikio ya msimu huu, Amini”

Mwanzo tu: Moyes akiingia uwanjani majira ya asubuhi kuendesha programu ya mazoezi

Yuko
fiti kurudi: Rio Ferdinand akiwasili uwanjani Carrington kufanya
mazoezi asubuhi ya leo kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka nchini
England

Nje: Rooney walivunja mawasiliano na Sir Alex Ferguson msimu uliopita, sasa msimu ujao atakubali kufanya kazi na David Moyes?


Kwenye rada
za watu: Rooney amekuwa akihusishwa kujiunga na Chelsea pamoja na
Arsenal katika majira haya ya joto ya usajili barani ulaya
0 comments:
Post a Comment