Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa wekundu wa Anfield au majogoo wa jiji, Brendan Rodgers amesisitiza kuwa mshambuliaji wake nyota Luis Suarez ataanza msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England akiwa mchezaji wa Liverpool , labda kama mambo mengine makubwa yatatokea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jakarta, kocha huyo ameweka bayana mipango yake kuwa ni kumbakisha nyota huyo raia wa Uruguay katika dimba la Anfield licha ya klabu za Arsenal na Real Madrid kumkodolea macho ya kuitaka saini yake.
Mapema wiki hii Mkurugenzi mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre, alithibitsha kuwa Arsenal ndio timu pekee iliyotuma ofa kwa Suarez, lakini kitita chao cha pauni milioni 30 kujumlisha tano walizoongeza ni ngumu kwa Liver kukubali kwani haiendani na thamani na jembe lao la ukweli.
Rodgers alisema kila wakati anawasiliana na Suarez na amekuwa akimueleza kuwa atajiunga na Liverpool wakati wa mchezo wao wa pili katika ziara yao wiki ijayo dhidi ya Melbourne, na katika mawasiliano hayo, kocha huyo ana imani kuwa nyota wake huyo mwenye umri wa miaka 26 ataendelea kubakia Anfield.
“Ni mchezaji wa ajabu,. Ni mchezaji wa Liverpool. Lakini haijalishi mchezaji ni mkubwa kiasi gani, hawazi kuwa mkubwa zaidi ya klabu ya Liverpool”. Alisema Rodgers.
“Luis ni mchezaji muhimu sana katika kikosi changu na naangalia namna ya kubaki naye msimu ujao. Kuna tetesi nyingi sana kuhusu yeye kuondoka, lakini bado naweza kusema ni mchezaji wa Liverpool”. Alisema Rodgers.
Sifa kubwa kuwa hapa: Liverpool wameanza ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England , Jakarta
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akiwa na bendera huko nchini Indonesia
Bado anajiamini sana: Rodgers amezungumza na wanahabari na kusema Luis Suarez ni mchezaji wa Liverpool na hataondoka kama tetesi zinavyosema
Akiwa katika dimbwi la mawazo: Rodgers jinsi alivyoonekana katika mazoezi ya Liverpool huko
Wakigongeana pasi kwa uzuri: Wacheaji wa Liverpool , akiwemo Steven Gerrard (kushoto) wakiwa katika mazoezi uwanja wa Gelora Bung Karno mjini Jakarta wakianza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England
Usinivute bwana: Fabio Borini (kshoto) na Martin Skrtel wakigombania mpira katika mazoezi ya Liverpool
Anawindwa ile mbaya: Luis Suarez amesema wazi kuwa anataka kuihama Liverpool
0 comments:
Post a Comment