Na Baraka Mpenja
Mabingwa wa soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam angalau leo hii wamepata cha kusema baada ya kupata sare ya 2-2 dhidi ya Wakusanyaji wa Mapato wa nchini Uganda, klabu ya URA, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga waliponea chupuchupu kulala kama wenzao Simba siku ya jana ambapo waliburuzwa 2-1 na wakali hao wa Uganda, lakini mshambuliaji ambaye hajaifungia Yanga kwa muda mrefu, Jerryson Tegete aliwapa cha kusema mashabiki wao baada ya kusawazisha bao la pili dakika ya 90 ya kipute hicho.

Dakika ya 61, Yayo alitikisa tena nyavu za wanajangwani na kuweka rekodi kufunga mabao manne ndani ya dimba bora la Taifa.
Katika dakika ya 69, Didier Kavumbagu aliisawazishia Yanga bao la kwanza baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa beki wa pembeni, Juma Abdul, na katika dakika ya 90 Tegete aliiokoa klabu yake baada ya kutia kambani gozi la ng`ombe.


Kizuguto alisema kocha wa klabu hiyo Ernie Brandts amesisitiza kuwa kikosi chake kimecheza vizuri, lakini wapinzani wake walikuwa wazuri sana.
Afisa habari huyo alisema kesho kikosi hicho kitakuwa na mapumziko, na kesho kutwa jumanne kitaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Loyola mabibo jijini Dar es salaam.
“Mechi ya leo ilikuwa nzuri sana kwa kikosi chetu, kocha amewapima wachezaji wake mbele ya timu nzuri, lakini sisi bado timu yetu ni nzuri sana”. Alisema Kizuguto.
Pia alisema hamasa ya mashabiki wa Yanga uwanjani imeonesha kuwa wanaipenda timu yao na wanatakiwa kuwa na moyo wa kuipenda zaidi kwani itawapa raha.
“Yanga ni timu ya wananchi,na ndio maana kila inapocheza wananchi wanajitokeza kwa wingi, hakika hatutawaangusha hata kidogo”. Alisema Kizuguto.
(PICHA ZOTE KWA HISANI YA MTANDAO)
0 comments:
Post a Comment