Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa
wa ligi kuu soka nchini Uingereza, mashetani wekundu Manchester United
leo hii wamepiga bonge la sherehe kushangilia ubingwa wao wa 20 pamoja
na kumuaga rasmi kocha wao aliyewafundisha kwa miaka 27 na kutwaa
makombe 49 katika michuano mbalimbali.
Viongozi,
wachezaji na mashabiki wa United leo hii wamepita mitaa mbalimbali ya
jijini Manchester kushangilia ubingwa wao na kumuaga Ferguson kwa
heshima kubwa.
Kocha
Kibabu leo hii kaagwa rasmi na kubwaga manyanga ya kuwanoa United na
kazi yake kumrithisha kocha ambaye amemhusudu kwa muda mrefu, David
Moyes ambaye kwa sasa ni kocha wa Everton.

Ferguson
amesitaafu huku akiwa tayari amesharejesha ubingwa alionyang`anywa na
watani zake wa jadi Manchester City msimu uliopita na kupeleka adhaa
kubwa kwa kocha wa City, Roberto Mancini ambaye kibarua chake kinaweza
kuinga mchanga wakati wowote baada ya kufanya vibaya msimu huu.
Feguson amekaa na timu kwa miaka 27, ni ngumu kujua kama Moyes ataweza kukaa muda kama wake akiwa na United ama la.
Watu wengi walidhani Mreno Jose Mourinho angebeba mikoba ya Fergie lakini imekuwa taofauti kabisa.

Gwaride la kashangilia ubingwa lilipita katika mitaa hiyo hapo juu

Mtoto akiwa ameshikilia bango lenye ujumbe kwa Wayne Rooney

Hana Furaha kabisa: Rooney alionekana kukosa furaha wakati akiwa katika basi leo

Mwisho: Mashabiki wa Manchester United wakijikusanya Albert Square kulisalimu basi la klabu yao

Asante sana: Shabiki mmoja Albert Square akisalimu picha ya Ferguson

Mashabiki wa United wakipeperusha bendera zao wakato wakisubiri basi la timu yao

ANAINGIA: Sir Alex Ferguson akiingia Old Trafford

Sir Bobby Charlton akijiunga na wachezaji wa United katika basi

Mkongwe Ryan Giggs akisaini katika vitabu vya kumbukumbu vya mashabiki wa united.

Shangwe ndio zinaanza kwa wachezaji wa United

Kombe: Robin van Persie akiinua juu taji lao la 20

Nani akiinua taji lao

Robin van Persie akiwapiga picha mashabki wa united





0 comments:
Post a Comment