Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
LEO 
NDIO LEO Uwanja wa Wembley Jijini London kuanzia Saa 3 Dakika 45Usiku 
wakati Klabu za Ujerumani , Mabingwa wa Nchi hiyo Bayern Munich na 
Mabingwa wa Msimu uliopita Borussia Dortmund, watakapocheza Fainali ya 
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ambapo Mshindi ndie rasmi Klabu Bingwa ya 
Ulaya.
Meneja
 wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp anaamini Fainali hii ya kwanza 
kuzikutansha Klabu za Germany ni kitu spesho na amesema: “Klabu hii 
ingeweza kusambaratika. Badala yake tumefufuka toka kwenye majivu. Hii 
ni Gemu spesho katika sehemu spesho dhidi ya Mpinzani maalum! Kama hii 
ndio Fainali yangu pekee maishani mwangu na nikifa nikiwa na Miaka 60 
basi haitakuwa mbaya!”
Klopp, akiongelea kusambaratika, alikuwa akimaanisha Mwaka 2005 ambapo nusura Klabu hiyo itangazwe mufilisi.
Borussia
 Dortmund watatinga Fainali hii bila Kiungo wao Chipukizi na hatari, 
Mario Gotze, ambae ni majeruhi lakini pia pengine hilo ni heri kwao 
kwani hii ingekuwa ni Mechi yake ya mwisho kwao kwani anahamia Bayern 
Munich kwa ajili ya Msimu ujao.
Akiongezea, Klopp, mwenye Miaka 45, alinena: “Soka ni Dini kwa Dortmund. 
Bayern
 Wanaweza kuwa na Mashabiki wengi na kushinda Mataji mengi, lakini sasa 
ni hadithi nyingine. Sasa imekuja Klabu nyingine ambayo ni nzuri pia. 
Tunazo pesa za kupata Wachezaji wazuri. Lakini zipo Klabu nyingine 
zinaweza kutumia pesa nyingi zaidi. Sisi tunachulkua msimamo tofauti!”
Lakini
 Kambi ya Mabingwa wa Germany, Bayern Munich, ipo na morali kubwa kupita
 Msimu uliopita walipofungwa Fainali ya UCL na Chelsea kwa Mikwaju ya 
Penati.
Mwaka 2010, Bayern pia walifungwa Fainali ya UCL na Inter Milan kwa Bao 2-0.
Akiongelea
 hali hii, Mchezaji wa Bayern, Thomas Muller, amesema: “Borussia ni Timu
 kamili. Hivyo ni ngumu kucheza nayo kupita Timu ya Wachezaji binafsi. 
Lakini sidhani kama tuna udhaifu. Tumecheza Gemu nyingi na hatujafungwa 
Bao nyingi. Ninajisikia vyema na nahisi tutapata matokeo mazuri!”
Kwenye
 Mashindano haya, Bayern wamesonga toka hatua ya Makundi kwa kishindo 
ingawa walisota walipocheza na Arsenal kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 
16 na kuitoa tu kwa Sheria ya Magoli ya Ugenini.
Lakini
 baada ya hapo walizisambaratisha Juventus na Barcelona kwa kuzinyuka 
Jumla ya Mabao 11-0 huku Barcelona wakitupwa nje ya Nusu Fainali kwa 
kutandikwa Bao 4-0 na 3-0 katika Mechi mbili.
 Ugeni:
 Kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp (kushoto) akiwa Wembley na kocha wa 
Aston Villa, Paul Lambert, ambaye aliiwezesha klabu hiyo ya Ujerumani 
kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 1997
 Tutawamaliza vipi?:Bastian Schweinsteiger, Arjen Robben na Franck Ribery wakiwa Wembley

 Anarekebishwa: Mshambuliaji tegemeo wa Dortmund, Robert Lewandowski akirekebishiwa viatu vyake
 Kiatu cha mabao: Kiatu cha Lewandowski fainali
 Utatu mtakatifu: Kevin Groskreutz, Robert Lewandowski na Marco Reus wakiwa mazoezini Wembley jana

0 comments:
Post a Comment