![]() |
PRISONS |
Na Baraka Mpenja, Dar es
Salaam
Ili kuhakikisha maafande wa jeshi la
magereza, Tanzania Prisons, “wajelajela” wanaibuka na ushindi wa nyumbani katika
mchezo wa keshokutwa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mgambo Jkt kutoka
mkoani Tanga, wadau na viongozi wa soka mkoani humo wamekutana kujadili namna ya kuisaidia timu hiyo.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya
simu, katibu mkuu wa Prisons, Sadick Jumbe, amesema wadau wamewafariji kwa
kiasi kikubwa na wameahidi kujitokeza kwa wingi kuwashangilia ili wapate
ushindi wa tatu nyumbani tangu waingie ligi kuu msimu huu.
“Kitendo cha wadau kukutana na sisi ni
uzalendo mkubwa sana, hii inaonesha upepo umebadilika kwa mashabiki wa jiji
hili, kama hali itaendelea kuwa hivi, lazima tuwatoe kimasomaso”. Alisema Jumbe.
Katibu huyo alisema maandalizi ya mchezo
huo yanakwenda vizuri, wachezaji wapo katika morali kubwa na mpaka sasa hakuna
mchezaji yeyote ambaye yuko hatarini kuukosa mchezo huo muhimu.
Kufuatia Prisons kutokuwa na rekodi
nzuri ya kushinda mechi za nyumbani, Jumbe
alisema kuwa sasa ni wakati wa kufuta makosa na kutumia vyema dimba la
nyumbani ambalo litasheheeni mashabiki lukuki.
“Kufungwa 1-0 mechi iliyopita na vijana
wa mitaa ya kishamapanda Toto Africans, ni sehemu ya mchezo, kama utakumbuka
tulijifunga, kama isingetokea vile tungetoa sare, lakini mwalimu umewapanga
vijana kisaikolojia ili kutumia nafasi ya nyumbani kupata ushindi”.
Wakati wajelajela wakijipanga kuwaadhibu
wapinzani wao, nao Mgambo JKT kupitia kwa katibu mkuu wake, Antony Mgaya,
wamesema wapo Mbeya kutafuta mzigo wa pointi tatu muhimu.
Mgaya alisema walifika mapema Mbeya ili
kuzoeza hali ya hewa mkoani humo ambayo alieleza kuwa kwa sasa kuna taofauti na
mikoa ya Pwani.
“Tuna kazi moja tu ya kuwafunga
wapinzani wetu ingawa watakuwa mbele ya mashabiki wao wenye hamasa kubwa,
lakini tumefanya mazoezi na kocha wetu Mohamed Kampira amefanya marekebisho
makubwa ya kikosi chake”. Alisema Mgaya.
Tanzania Prisons wapo nafasi ya 11
wakiwa na ponti 20 kibindoni wakati Mgambo JKT wapo katika nafasi ya 9
wakijikusanyia pointi 24 kibindoni.
Ushindani wa mechi hiyo unatarajiwa kuwa
mkubwa kutokana na timu zote kuwa miiongoni mwa klabu zinazohitaji kujinasua na
mstari mwekundu wa kuporomoka daraja.
![]() |
MGAMBO JKT |
0 comments:
Post a Comment