KLABU ya Chelsea imetinga Nusu Fainali 
ya Kombe la FA baada ya kuilaza bao 1-0 Manchester United jioni hii 
kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London. 
Ushindi huo umetokana na bao pekee la Demba Ba dakika ya 49 akimaliia kazi nzuri ya Juan Mata. 
Javier Hernandez alipata nafasi nzuri ya
 kuisawazishia United, lakini mpira wake alioupiga kwa kichwa uliokolewa
 na kipa wa Chelsea, Petr Cech. 
Robin van Persie aliyeingia kutokea 
benchi naye alipata nafasi ya kuisawazishia United lakini, shuti lake 
akiwa umbali wa mita sita liliota mbawa. 
Kwa ushindi huo, The Blues sasa watamenyana na Manchester City kwenye Uwanja wa Wembley kuwania kutinga Fianali.
Katika mchezo huo, kikosi cha Chelsea 
kilikuwa: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole/Bertrand dk22 Mikel, 
Ramires, Hazard, Mata, Oscar/Moses dk90 na Ba/Torres dk90
Manchester United:
 De Gea; Jones, Smalling, Ferdinand, Evra, Valencia, Carrick, 
Cleverley/Van Persie dk61, Nani/Giggs dk65, Hernandez na Welbeck/Young 
dk80.

Shuti la bao: Demba Ba akiifungia Chelsea bao pekee la ushindi

Cheki kitu hicho: Demba Ba akifunga na chini akishangilia bao lake
 .


Yamekwisha: Rio Ferdinand, ambaye alizomewa na mashabiki wa Chelsea, hapa anapeana mkono na Ashley Cole.

0 comments:
Post a Comment