
Ligi kuu
soka visiwani Zanzibar imeendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa.
Klabu ya
Chipkizi imewakung`uta Malindi mabao 2-1 na kupata pointi tatu muhimu.
Katibu mkuu wa chama cha soka visiwani Zanzibar
ZFA Masud Ettei, amesema mchezo huo ulikuwa wa kukata na shoka kutokana na timu
hizo kuhitaji pointi tatu muhimu wakati huu ambapo ligi hiyo ipo mwishoni.
Ligi hiyo
itaendelea kesho kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti.
Kisiwani Pemba
vinara ligi hiyo KMKM wakiwa na poniti 45 watashuka dimbani kugagaduana klabu ya Jamhuri, wakati huo huo Kisiwani Unguja Zimamoto watakabiliana na Mafunzo wanaowania nafasi ya
kutwaa taji la ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment