>>RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16 YAANZA!!
+++++++++++++++++++
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumanne 12 Februari 2013
Celtic v Juventus
Valencia v Paris St Germain
+++++++++++++++++++
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya
Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI inaanza leo kwa Mechi mbili za kwanza
kati ya Celtic v Juventus na Valencia v PSG na pia itaendelea kesho kwa
Mechi mbili kati ya Real Madrid v Manchester United na Shakhtar Donetsk v
Borussia Dortmund.
Raundi hii itakamilisha Mechi zake za kwanza Wiki ijayo na Marudiano yatachezwa kuanzia Machi 5.
CELTIC v JUVENTUS

HALI za TIMU:
Celtic wana wasiwasi kuhusu Wachezaji
wao wawili, Georgios Samaras na Efe Ambrose, ambao wana maumivu na
uchovu hivyo watachekiwa leo kujua kama wataivaa Juventus au la.
Wakati Samaras ana matatizo ya Musuli za
Mguu, Efe Ambrose aliichezea Nigeria kwenye Fainali ya AFCON 2013 juzi
Jumapili walipotwaa Ubingwa kwa kuifunga Burkina Faso Bao 1-0 hivyo
atachelewa kurudi Mjini Glasgow.
Kwa upande wa Juventus, Kiungo Kwadwo
Asamoah nae alikuwa huko Afrika Kusini kwenye AFCON 2013 alipoichezea
Ghana hivyo huenda asicheze Mechi hii.
NYOTA WA TIMU:
-CELTIC: Samaras
-JUVENTUS: Pirlo
NINI WAMESEMA MAMENEJA:
Meneja wa Celtic Neil Lennon: "Tuna
wasiwasi na Wachezaji wetu kadhaa lakini tuna Timu nzuri. Kuifunga
Barcelona hapa na kididogo tuifunge huko Nou Camp inathibitisha hilo.
Meneja wa Juventus Antonio Conte: "Sisi
hatuwadharau Celtic. Tumewaangalia sana na walikuwa imara walipocheza
na Spartak, Benfica na Barcelona. Ni Timu nzuri. Kuifunga Barca
inathibitisha hilo!”
VIKOSI VINAVYOWEZA KUAANZA:
Celtic
Kipa: Forster
Mabeki: Matthews, Lustig, Wilson, Izaguirre
Viungo: Brown, Wanyama, Mulgrew
Washambuliaji: Samara, Hooper, Forrest
Juventus
Kipa: Buffon
Mabeki: Bonucci, Barzagli, Caceres
Viungo: Lichsteiner, Marchisio, Pirlo, Vidal, Asamoah
Washambuliaji: Vucinic, Giovinco
VALENCIA V PARIS ST-GERMAIN
UWANJA: Mestalla, Valencia, Spain
HALI za TIMU:
PSG itawakosa Beki Thiago Silva na
Kiungo Thiago Motta kwa vile ni majeruhi na pia Mchezaji mpya David
Beckhan, ambae ingawa amesafiri na Timu, hatawekwa kwenye Kikosi
kitakachocheza na Valencia.
Valencia hawana Majeruhi na juzi
waliwapumzisha kwenye Mechi ya La Liga dhidi ya Celta Vigo Wachezaji wao
Joao Pereira, Victor Ruiz na Diego Alves ili wawe freshi kwa ajili ya
Mechi hii.
NYOTA WA TIMU:
-VALENCIA: Roberto Soldado
-PSG: Zlatan Ibrahimovic
NINI WAMESEMA MAMENEJA:
Paris St-Germain manager Carlo Ancelotti: “Valencia ni Timu nzuri sana. Wanacheza
staili ya Spain ya kupanda juu na pasi fupi fupi. Wakiwa na Soldado
wapo hatari sana kwani hutoka nyuma na kupanda kwa kasi sana”
Valencia head coach Ernesto Valverde: “Tunapitia kwenye hali nzuri Kitimu na tupo kwenye morali nzuri. Gemu kama hizi ni nafasi nzuri kwetu.”
VIKOSI VINAVYOWEZA KUANZA:
Valencia (Mfumo 4-2-3-1):
Kipa:Vicente Guaita
Mabeki: Andres Guardado, Adil Rami, Ricardo Costa, Joao Pereira
Viungo: Victor Ruiz, Tino Costa; Jonas, Ever Banega, Sofiane Feghouli
Mshambuliaji: Roberto Soldado
Paris Saint-Germain (Mfumo 4-2-3-1):
Kipa: Salvatore Sirigu
Mabeki: Maxwell, Mamadou Sahko, Alex, Cristophe Jallet
Viungo: Blaise Matuidi, Marco Verratti; Ezequiel Lavezzi, Javier Pastore, Lucas Moura
Mshambuliaji: Zlatan Ibrahimovic
+++++++++++++++++++
RATIBA-MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumatano 13 Februari 2013
Real Madrid v Manchester United
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
Jumanne 19 Februari 2013
Arsenal v Bayern Munich
FC Porto v Malaga
Jumatano 20 Februari 2013
Galatasaray v FC Schalke
AC Milan v Barcelona
MARUDIANO
Jumanne 5 Machi 2013
Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk
Man United v Real Madrid
Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic
Paris St George v Valencia
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
0 comments:
Post a Comment