Ligu kuu Tanzania
bara inaendelea leo kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali.
Wakata miwa wa Kagera
sugar wapo nyumbani kuvaana na wagosi wa kaya, klabu ya coastal union kutoka
jijini Tanga katika uwanja wa kaitaba mkoani kagera.
Watoto wa mitaa ya
kishapanda jijini Mwanza, klabu ya Toto African ni wenyeji wa polisi morogoro
katika uwanja wa CCM Kirumba mwanza.
Mgambo shooting
wamewakaribisha JKT Oljoro kwenye uwanja wa ccm mkwakwani mkoani Tanga.
Mtibwa sugar wapo
yumbani manungu complex kuvaana maafande wa jeshi la kujenga taifa, Ruvu
shooting kutoka mkoani Pwani.
YANGA inashuka
uwanjani leo uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuikabili African Lyon.
 
 LakiniÂ
Azam inampa presha kubwa kocha Ernest Brandts ambaye ameagiza wachezaji
wake kuhakikisha wanaishushia mvua ya mabao Lyon ili kuwadhibiti wana lamba lamba hao.
 Azam
iliibamiza Mtibwa Sugar Jumapili ya wiki
iliyopita mabao 4 – 1 na kukabana koo na Yanga kileleni.
 Timu zote hizo zina pointi 33, lakini Yanga inaongoza kwa tofauti ya
mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba bado inachechemea katika nafasi ya tatu baada ya kulazimishwa
sare ya bao 1 – 1 JKT Oljoro Jumamosi iliyopita jijini Arusha.
 Brandts
amesema kuwa ligi sasa imefikia patamuÂ
na hakuna kudharau timu hata moja ingawa kasi wanayokuja nayo Azam ni
kubwa na inamuogopesha katika harakati zao za kutwaa ubingwa ingawa amedai
kuwa atawatuliza tu na Yanga itakuwa
bingwa msimu huu.
Kocha huyo raia wa
Uholanzi amewaambia wachezaji wake wajifunze kutokana na matokeo wanayopata
Simba hivi sasa kwa kutambua kuwa sasa
ni muda wa kazi na wanatakiwa kujituma
zaidi ili kusaka mafanikio.
 Vita ya
ubingwa imeonekana kupamba moto katika
timu tatu Yanga, Azam na Simba ingawa wekundu hao wa Msimbazi wameonekana
kuchechemea katika mbio hizo.
 Ingawa Yanga
inaonekana ina ahueni zaidi katika
michezo yake 11 iliyobaki kwani mechiÂ
sita ndio zinaonekana zitaipa shida timu hiyo katika harakati zake za
kuwania ubingwa wakati Azam ina mechiÂ
saba ngumu pia wakati Simba ndio ina kazi kubwa zaidi kwani ina
mechi tisa ngumu.
 Yanga ina
mechi ngumu dhidi ya JKT Ruvu, Azam,
Kagera Sugar, JKT Oljoro, Coastal Union na Simba ingawa inapata haueni kwani mechi nyingi inacheza
kwenye Uwanja wa nyumbani wakati Azam ina kazi dhidi ya JKT Ruvu, Yanga, Ruvu Shooting, Simba, Coastal na Oljoro na
Mgambo Shooting.
 Simba yenyewe
itabidi ifanye kazi ya ziadaÂ
kuziadabisha Prisons, Ruvu
Shooting, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Kagera, Azam, Toto, Mgambo Shooting na Yanga.
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
PTS
|
1
|
YANGA
|
15
|
10
|
3
|
2
|
17
|
33
|
2
|
AZAM
FC
|
16
|
10
|
3
|
3
|
13
|
33
|
3
|
SIMBA
|
16
|
7
|
7
|
2
|
11
|
28
|
4
|
COASTAL
|
16
|
7
|
6
|
3
|
4
|
27
|
5
|
RUVU
SHOOTING
|
15
|
7
|
3
|
5
|
3
|
24
|
6
|
KAGERA
|
16
|
6
|
6
|
4
|
2
|
24
|
7
|
MTIBWA
|
16
|
6
|
5
|
5
|
2
|
23
|
8
|
JKT
OLJORO
|
16
|
5
|
6
|
5
|
1
|
21
|
9
|
MGAMBO
|
16
|
5
|
3
|
7
|
-6
|
18
|
10
|
PRISONS
|
16
|
4
|
6
|
6
|
-6
|
17
|
11
|
JKT
RUVU
|
15
|
4
|
4
|
7
|
-8
|
16
|
12
|
TOTO
|
16
|
2
|
7
|
7
|
-9
|
13
|
13
|
POLISI
|
15
|
2
|
4
|
9
|
-10
|
10
|
14
|
LYON
|
16
|
2
|
3
|
10
|
-16
|
9
|
0 comments:
Post a Comment