Wednesday, January 30, 2013


Baada ya kuvuliwa ubingwa wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kutoka sare na Burkinafaso, Zambia wanaamini bado inawezekana kwao kufuzu fainali za kombe la dunia 22014 hivyo wachezaji wa kikosi hicho wanatakiwa kuaminiwa na kuepuka kubadilisha kikosi hicho baada ya kutolewa hatua ya makundi ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON.

Kocha wa Chipolopolo mfaransa, Herve Renard amesema licha ya Zambia kutolewa hatua ya awali ya AFCON, kufuzu kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil ndio imebaki kazi kubwa kwao.

Renard amesema Zambia walikuwa na malengo mawili, moja ilikuwa  ni kutetea ubingwa wao wa AFCON pili kufuzu fainali za kombe la dunia, wameshindwa la kwanza na sasa bado wana nafsi ya kujipanga kufuzu kombe la dunia.

Kocha huyo aliongeza kuwa kuwepo kundi moja na Ghana kuwania kufuzu kombe la dunia haitakuwa rahisi kwao lakini watajipanga kwani walianza vizuri michezo ya kwanza.


Kocha huyo alisistiza kuwa Zambia watacheza na Lesotho ugenini halafu watakutana nao kwao Lusaka juni mwaka huu, halafu watacheza nyumbani na Sudan na mwisho watavaana na Black stars Ghana wakiwa ugenini mjini Accra mechi ambayo itakuwa kama fainali.

Zambia mpaka sasa wana pointi 6 walizopata baada ya kushinda mchezo mmoja na kupewa poniti za 3 za bure kutoka kwa Sudan walioadhibiwa na FIFA kwa kosa la kumtumia mchezaji aliyesimamishwa.

Kuhusiana na kibarua chake, Renard alisema Zambia sio kama mataifa ya mengi ya afrika ambayo hukimbilia kuwatimua makocha, lakini Rais wa chama cha soka Zambia Kalusha Bwalya ana maarifa makubwa katika soka,  ila kama watamtaka kuondoka atakubali na wanatakiwa kukaa naye na kula chakula cha mchana pamoja na kumwambia aende na yeye atafunga virago vyake na kurudi nyumbani bila tatizo lolote.

Renard aliwapa Zambia ubingwa wa kombe la mataifa mwezi februari mwaka jana bila matarajio.
Zambia hawajawahi kufuzu fainali za kombe la dunia.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video