Tuesday, January 22, 2013

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa amewataka wadau
wote wa maendeleo ya mkoa wa Mtwara kusitisha harakati zao za
maandamano na mihadahara ya kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha
gesi kwenda Dar es salaam na badala yake kukaa pamoja kujadili suala
hilo

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari,imemnukuu rais Mkapa
akizitaka pande zote kushirikiana kwa pamoja kupitia
historia,kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wa mradi huo na na
kufikia muafaka wa ujia wa maendeleo

Rais Mkapa amesema fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano kamwe si
masharti ya maendeleo bali mazungumzo yataboresha sera, ya uwekezaji
ya mkoa na nchi kwa ujumla.


Amesema vituko na kauli za hivi karibuni kutoka kwa wananchi na
viongozi wa vyama vya siasa  zimekaribia kujenga kutokuelewana kati ya
Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali, kati ya wanachama wa vyama
vya siasa na viongozi wao, kati ya wananchi na viongozi wa Serikali.

Ameongeza kuwa Mtafaruku huu haufai kuachwa uendeleee na kutishia
usalama kwa kuwa mipango,  Mikakati na mbinu za Utekelezaji wa
maendeleo siyo siri na kwamba maelezo yake mazuri yanaweza kutolewa
yakadhihirisha namna na kasi ambayo raslimali zitawanufaisha wananchi
wa eneo hilo

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video